Pages

Sunday, July 22, 2012

BI. HARUSI AFA BWANA HARUSI APONA



HUKU majonzi yakiwa bado yametawala miongoni mwa Watanzania kufuatia vifo vya watu waliokuwa ndani ya meli ya MV Skagit ambayo ilipinduka na kuzama Julai 18, 2012 karibu na Kisiwa cha Chumbe, Zanzibar mambo mengi yameibuka.

Nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik siku ya Jumatano (juzi) ambako serikali ilikuwa ikitoa ripoti ya maendeleo ya uokoaji, baadhi ya watu walikuwa katika hali ya majonzi kufuatia ndugu zao kutojulikanna walipo.
Hamis, aliyedai ni mfanyakazi wa Kampuni ya Azam ya tajiri Said Salim Bakheressa alisema mdogo wake, Khalfan na mchumba wake, Zaina Ally walikuwa ndani ya meli hiyo kwenda Zanzibar kufunga ndoa Alhamisi (juzi) kama maandalizi ya kuukaribisha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, lakini mpaka siku hiyo mdogo wake aliokolewa, ila Zaina hajulikani alipo.
Hamis alisema: “Naamini shemeji yangu amefariki dunia, kwani katika watu wote waliokolewa hayupo, maskini mdogo wangu (Khalfan), alikuwa akafunge ndoa ili wakati wa swaumu mkewe awe halali kumpikia chakula.”
Akaongeza: “mbaya zaidi, mpaka muda huu (saa saba mchana Alhamisi) serikali imetangaza kupatikana kwa miili mingine nane, lakini pia shemeji yangu hayupo.”
Hamis aliongeza kuwa ndoa hiyo ilikuwa ifungwe jijini Dar wiki iliyopita, lakini wazazi wa Zaina ambao wote wanafanya kazi serikalini Zanzibar waliomba ikafungwe visiwani humo.

MENGINE YA KUSHANGAZA
Mtu mwingine ambaye hakutaja jina lake, alisema siku ya tukio, yeye alimsindikiza mdogo wake mpaka bandarini, akiwa anapanda meli hiyo, yeye akaondoka kuendelea na shughuli zake.
“Sasa niliposikia meli imezama, nikampigia simu, hakupatikana, nikajua tayari. Nilituma habari kwa ndugu mbalimbali tayari kwa maandalizi ya msiba.

“Lakini ilipofika saa kumi na mbili jioni akanipigia simu akiniuliza kama nimesikia kuna meli imezama. Nilishtuka, nikahisi naongea na mzimu, nilipomuuliza ameponaje akasema alighairi akapanda meli nyingine, alipofika Zanzibar simu yake ikazima kwa sababu ya kuishiwa chaji.”

Naye mzee Fasha Abduel, mkazi wa Magomeni, jijini Dar, alisema siku hiyo ya tukio, asubuhi alimpeleka bandarini mtoto wa mdogo wake aitwaye Shaban na alimkatia tiketi kwenye meli hiyo, lakini kijana huyo alikuwa hataki kwenda Zanzibar ambako ndiko aliko baba yake mzazi.
“Kumbe nilipoondoka kwenda kazini kwangu (Manispaa ya Temeke) na yeye akageuza kurudi nyumbani. Ajali ilipotokea nilishtuka sana, nikampigia simu mdogo wangu kule Zanzibar, akaanza kilio. Nilipompigia mke wangu kumjulisha, akasema mbona Shaban alirudi muda uleule wa asubuhi na amejaa tele nyumbani,” alisema mzee huyo.

Mzee Hassan, mkazi wa Kariakoo, jijini Dar, yeye alikuwa akipeleka magunia matupu Zanzibar, lakini asubuhi wakati akijiandaa, mwanaye wa kiume, Ally anayesoma Shule ya Msingi Makurumla, Dar aliugua ghafla, hivyo ikabidi yeye akatume magunia hayo kwenye meli hiyo na kumtaarifu mtu wa kuyapokea Bandari ya Malindi, Zanzibar ikawa salama yake.

HALI HALISI
Mpaka tunakwenda mitamboni, maiti zilizopatikana kufuatia ajali hiyo ni 31 huku 146 wakiwa wameokolewa na 117 hawajulikani walipo.
MELI YAFIKA MITA 47
Habari zaidi zisema kuwa, meli hiyo ambayo ilizama jumla jioni ya Jumatano, ilifika kina cha mita 47 kwenda chini wakati uwezo wa wazamiaji waliokuwa kwenye eneo la tukio ni mita 30 tu.
SPIKA WA BUNGE AWARUHUSU WABUNGE KWENDA MISIBANI
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda, Julai 19, aliahirisha bunge na kuwataka waheshimiwa waende misibani kuungana na Watanzania wengine katika kipindi hiki kigumu.
SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO ZAISHA LEO
Wakati serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ikitangaza siku tatu za maombolezo ambapo bendera hupepea nusu mlingoti, juzi Alhamisi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano nayo ikatangaza siku tatu za maombelezo kwa nchi nzima ambazo zinakwisha leo.

KWA NINI KUTOKA DAR?
Kumbukumbu za haraka zinaonesha kuwa, sehemu kubwa ya ajali za meli hutokea wakati wa kutoka Dar kwenda Unguja au Pemba.
Miezi kumi iliyopita, Meli ya MV Spice Islanders ilipata ajali ikiwa inatoka Dar, kupitia Unguja kwenda Pemba.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema hata meli nyingi zinazozima injini majini, nyingi huwa zinatoka Dar kwenda Unguja.

UITABIRI WA MAAFA KUONGEZEKA
Wakati hayo yakitokea, baadhi ya Watanzania wametabiri ajali zaidi za meli wakidai kuwa nyingi haziko vizuri kwa safari za majini.
“Kama serikali haitachukua hatua ya kukagua meli zetu, ajali nyingi mbele zinakuja kwani meli nyingi hazina sifa ya kufanya safari za majini kutokana na kuzeeka au kutofanyiwa matengenezo.
KUTOKA KWA MHARIRI
Mungu awatie nguvu na uvumilivu wale wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo. Tuliwapenda wapendwa wetu, lakini Mungu amewapenda zaidi. Amina.

Friday, July 20, 2012

MAMA KANUMBA AMVAA MAMA LULU

CHOKOCHOKO zimeanza! Huku kesi ya kifo cha mwanaye ikiendelea na Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akisota nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea, mama mzazi wa marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Flora Mtegoa amemvaa mama Lulu, Lucresia Karugila, Ijumaa linafunguka.
MANENO MAZITO YA AIBU
Kwenye mahojiano maalum na gazeti hili nyumbani kwake Kimara-Temboni, Dar es Salaam, mapema Jumanne wiki hii, mama Kanumba alimtolea mama Lulu maneno mazito huku akimshangaa kwa kushindwa kumpa pole na kumfariji tangu mwanaye afikwe na umauti Aprili 7, mwaka huu.
Mama Kanumba alisema anaongea kwa uchungu kwani hakutegemea kama mama Lulu anaweza kuwa kimya mpaka leo hii bila hata kumpa pole wakati matatizo yamewakuta watoto wao wote.
TUPATE SAUTI YA MAMA KANUMBA
Ijumaa: Ili kupata kile alichokisema mzazi huyo mbele ya gazeti hili, tujiunge naye akiwa nyumbani kwake Kimara-Temboni.
Kwako mama Kanumba: Namshangaa sana mama Lulu kwani namuona kama siyo mzazi mwenzangu. Huwezi amini mpaka leo hii hajawahi hata kunipa pole wala kunitumia ujumbe wa watu kunifariji, hivi anategemea mimi nimfuate? Yeye mwanaye yupo hai wangu ndiyo ametangulia. Nimeona niseme kabisa nimpe habari yake.
Ijumaa: Kwani wewe uliwahi kufanya jitihada za kukutana na kufarijiana naye akakataa?
Mama Kanumba: Mama Lulu siyo kabisa. Aliwahi kufuatwa na kuombwa ushirikiano wakati kesi imefunguliwa akakataa.
Ijumaa: Mbona kuna madai kuwa baada ya kifo cha Kanumba upande wa Lulu ulikufuata ukakataa kutoa ushirikiano?
Mama Kanumba: Sijawahi kuongea na mtu yeyote wa upande wa Lulu. Huyo anayedai alikuja kuniomba ushirikiano nikamfukuza ananisingizia kwani simfahamu Lulu na mama yake zaidi ya kuwaona kwenye vyombo vya habari na filamu (Lulu).
Ijumaa: Je, akikufuata utamkubalia aje kukufariji?
Mama Kanumba: Mimi sina nia mbaya na mama Lulu, kibinadamu namuona kakosea kwani kama yeye alikuwa akiogopa, angetuma watu waje kwa niaba yake. Nilidhani alikuwa akiogopa kuja Sinza (Vatican kwa Kanumba) kwa sababu ya waandishi lakini hata nilipohamia huku (Temboni) hajaja. Ukweli ni kwamba akija nitampokea tu ila sidhani kama ipo siku atakuja, nawashangaa hata washauri wake.
Ijumaa: Unaizungumziaje filamu ya Foolish Age ya Lulu ambayo Kanumba aliipeleka Steps?
Mama Kanumba: Ni kweli filamu hiyo ipo Steps, Kanumba ndiye aliipeleka kwa nia ya kumuinua Lulu lakini kabla haijalipwa mauti yakamkuta. Ingekuwa ya Kanumba ningefuatilia.
Baada ya mahojiano hayo, Ijumaa lilitafuta mzani upande wa pili wa mama Lulu ambapo mahojiano yalikuwa hivi:
TUJIUNGE NA MAMA LULU AKIWA TABATA
Ijumaa: Mama Lulu gazeti la Ijumaa limezungumza na mama Kanumba anakulaumu kwa kushindwa kumfariji baada ya kifo cha mwanaye Kanumba aliyekutwa na umauti akiwa na Lulu. Je, unalizungumziaje suala hili?
Mama Lulu: Eehee unasemaje? Wewe ni nani? Mwandishi? Nimeshawaambia mniache kabisa kwani bila habari ya Lulu na Kanumba hamuuzi?
Ijumaa: Katika maadili ya kazi yetu mtu mmoja akiongea lolote juu ya mwenzake lazima pande zote zisikilizwe hivyo hii ndiyo nafasi yako. Unalizungumziaje suala hilo la mama Kanumba?
Mama Lulu: Sitaki kushauriwa na wewe mwandishi, nina washauri wazuri tu tena ni watu wazima, tafadhali naomba mniache nipumzike.
KIFUATACHO
Bado kesi ya Lulu ni mbichi ambapo itaendelea kuunguruma baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumaliza utata wa umri na jina la Lulu Julai 23, mwaka huu.
KALAMU YA IJUMAA
Wazazi hawa wanapaswa kuwa na staha kwa sababu kila upande una machungu. Kanumba hatunaye na Lulu yupo nyuma ya nondo. Ni vyema wakakaa chini bila kukorogana ili kupunguza machungu waliyonayo.

WEMA, DIAMOND WANASWA KIGOMA

Nasib Abdul Juma ‘Diamond’.

STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma ‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma, Ijumaa lina data kamili.

Chanzo makini kilichopo mkoani humo, kimepenyeza habari hiyo kwa paparazi wetu kwa njia ya simu juzi, ambapo kilisema ukaribu wao uliamsha hisia kwamba huenda wawili hao wamerudiana.

“Wapo wote huku…
Nasib Abdul Juma ‘Diamond’.
Wema Isaac Sepetu.
STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma ‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma, Ijumaa lina data kamili.
Chanzo makini kilichopo mkoani humo, kimepenyeza habari hiyo kwa paparazi wetu kwa njia ya simu juzi, ambapo kilisema ukaribu wao uliamsha hisia kwamba huenda wawili hao wamerudiana.
“Wapo wote huku Kigoma, kwa Diamond ni sawa maana yupo na wasanii wenzake wa Kigoma All Stars, sasa Wema amekujaje? Kwanza siyo mwanamuziki, lakini pia siyo mtu wa Kigoma ni wa kutoka Tabora,” kilieleza chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hiyo, Ijumaa lilimvutia waya Diamond zaidi ya mara tatu lakini simu iliita bila kupokelewa.
Wema alipopigiwa simu alipatikana na kufafanua ishu nzima ilivyo. Huyu hapa msikie: “Ni kweli nipo huku Kigoma lakini sipo na Diamond. Nimekuja kwa mwaliko wa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini).
“Mimi na Diamond ni marafiki tu, hatuwezi kuwa wapenzi tena, kila mtu na maisha yake. Kifupi nina mtu wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana.”
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake mpya alisema: “Kwa sasa siwezi kumtaja, lakini siku si nyingi nitamuweka hadharani watu wamjue.”

Saturday, July 14, 2012

NI VITA...




MCHEZO ULIVYOANZA
Akizungumza na…



MCHEZO ULIVYOANZA
Akizungumza na mapaparazi wetu juzikati, jijini Dar, Mchungaji Mwamkamba alisema awali alitoa matangazo na pia kutuma ujumbe mfupi wa simu ‘SMS’ kwa watu mbalimbali akiomba mchango wa fedha ili aweze kujenga kanisa lake, lakini bila matarajio yake, namba zake ziliangukia mikononi mwa watu hao.
“Nilitarajia kupanua kanisa langu hivyo nilihitaji mchango wa fedha kwa ajili ya ujenzi, nikatoa tangazo kwa watu mbalimbali pamoja na kutuma SMS kwa marafiki zangu.
“Siku moja nilipigiwa simu na watu nisiowajua, wakaniambia wanataka kukutana na mimi ili wanisaidie fedha  za ujenzi wa kanisa langu.
“Nilikubali, nikaenda kukutana nao pale Ubungo. Walianza kunieleza jinsi walivyoamua kunisaidia kujenga hekalu la Mungu huku wakisema wananipa fedha za kutosha na kuagana na umaskini,” alisema Mchungaji Mwamkamba.
Aliendelea kudai kuwa watu hao walisema lengo lao ni kumpa kiasi chochote cha fedha ambacho kilikuwemo kwenye ‘brifkesi’ kwa ajili ya ujenzi huo.
“Waniliambia wananipa kiasi chochote cha fedha ninachokihitaji, lakini iwe siri yangu na wao, halafu wakasema waumini katika kanisa langu wataongezeka.

MCHUNGAJI AZIDI KUFICHUA
“Wakaniambia wamefanya hivyo kwa watumishi wengi wa Mungu hapa Tanzania ambao kwa macho ya kawaida huwatambuliki kama ni wafuasi wa Freemason na wanafanya ishara na miujiza mingi huku makanisa yao yakiwa na idadi kubwa ya waumini.”
APEWA MKATABA
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na kabla mchungaji huyo hajasema ndiyo au hapana, alipewa mkataba wenye maelekezo ya jinsi ya kujiunga ili aanze kula mema ya nchi na kuuaga umaskini kwa muda mfupi.
“Walinipa mkataba, una nembo ya Freemason, lakini wakaniambia ni lazima nibadili dini, nianze kuvaa nembo ya mwewe na nyoka na kumtoa kafara mke wangu au mwanangu nimpendaye kama sadaka ya shukrani kwa mungu wao,” alisema mchungaji.
AWACHOMOLEA WAZI
“Niliposikia masharti hayo, ghafla nilisikia uchungu moyoni, nikakataa, nilisimama haraka sana na kuondoka kwa mwendo wa haraka, kama nakimbia. Wakaanza kunizomea huku wakitoa ishara ya kuvunja vidole viwili ambayo ni moja ya alama za Freemason,” alisema mchungaji huyo.
KWA NINI NI VITA?
Hivi karibuni, Mchungaji wa Kanisa la Good News for All Nations, Mark Diganyeka alitoa alama za kuwatambua watumishi wa Mungu ambao ni waumini wa dini ya Freemason na kusema kuwa waumini wawe makini kuwabaini.
Miongoni mwa alama hizo alisema ni pamoja na kuvunja vidole kwa haraka wakati wakihubiri na kuvaa pete kubwa kwa ajili ya kufanyia miujiza wawapo madhabahuni.
Kwa tafsiri ya Mchungaji Diganyeka na hayo aliyokutana nayo Mchungaji Mwamkamba, ni dhahiri  makanisa yameingiliwa na Freemason hivyo kuanza kutimia kwa yale maneno kwamba, imani hiyo itawavaa watumishi wa Mungu kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo.

AIBU TUPU...



Ni aibu tupu! Mnyange aliyeibuka mshindi wa pili kwenye kipute cha Miss Vyuo Vikuu au Miss Higher Learning 2012/13, Fatma Ramadhan (pichani), ameacha gumzo baada ya kukwea jukwaani akiwa kaacha wazi mlango wake wa ‘ikulu’ bila kufuli, Risasi Jumamosi linairusha hewani.
NI MBELE YA MBUNGE

Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na mwandishi wetu, lilijiri usiku wa kuamkia Julai 7, mwaka huu kwenye Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki, Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Kisesa kwa leseni ya CCM, Mhe. Luhaga Joelson Mpina.
Katika…


Ni aibu tupu! Mnyange aliyeibuka mshindi wa pili kwenye kipute cha Miss Vyuo Vikuu au Miss Higher Learning 2012/13, Fatma Ramadhan (pichani), ameacha gumzo baada ya kukwea jukwaani akiwa kaacha wazi mlango wake wa ‘ikulu’ bila kufuli, Risasi Jumamosi linairusha hewani.
NI MBELE YA MBUNGE
Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na mwandishi wetu, lilijiri usiku wa kuamkia Julai 7, mwaka huu kwenye Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki, Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Kisesa kwa leseni ya CCM, Mhe. Luhaga Joelson Mpina.
Katika tukio hilo ambalo hata mheshimiwa mbunge aliliona na kutazama pembeni, ilifahamika kuwa mrembo huyo aliyetimba jukwaani akiwa hajavaa nguo ya ndani, alitokea kwenye Chuo Cha Uandishi wa Habari mkoani Arusha.
“Jamani… jamani! Yaani huyu binti yuko uchi kabisa, imekuwaje au kajisahau? Ni aibu iliyoje, tena mbele ya mheshimiwa mbunge? Hii kweli aibu tupu,” alisikika mmoja wa watazamaji wa kinyang’anyiro hicho.
RASHIDA NAYE AANIKA MAMBO
Katika tukio lingine la aibu kwenye ‘iventi’ hiyo, kivazi cha mkufunzi wa warembo ambaye ni Miss Mara 2000, Rashida Wanjara kiliacha watu midomo wazi baada ya kuanika mambo yake nyeti ya mwilini.
“Duh! Huyu naye kiboko. Yaani kila kitu mpaka vya chumbani kaviacha hadharani?”
HEBU MSIKIE
Risasi Jumamosi lilipomvaa na kumuuliza kulikoni kuvaa kigauni kinachoonesha maungo yake nyeti, alifunguka: “Mimi ndiye miss nisiyechuja, nikiamua kushiriki umiss bado nakubalika na mwili wangu unalipa.”

AFANDE SELE AKIFUNGUKA KUHUSU SHOW YA ZANZIBAR MUSIC AWARD

Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
"Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma "MBELE YAKO NYUMA YANGU" .. Kuna mstari Nilisema " ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu".
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)
 

Blogger news

Search This Blog

Blogroll

Follow by Email

About